RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Mapinduzi ya Januari 12, 1964 yameleta usafiri wa uhakika wa barabara bora mjini na vijijini hapa Zanzibar. Rais Dk. Shein aliyasema hayo leo katika uzinduzi wa Barabara ya Kijitoupele hadi Fuoni Mambosasa huko katika uwanja wa Mzee Mgeni Fuoni Mambosasa Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi, ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi.
Katika maelezo yake, Rais Dk. Shein alisema kuwa baada ya Mapinduzi matukufu ya Januari 12, 1964 mipango ya maendeleo ndipo iliopoanza ikiwa ni pamoja na kujenga barabara zilizo bora. Rais Dk. Shein alisema kuwa kabla ya Mapinduzi hapakuwa na barabara zenye hadhi na kiwango cha ubora kama ilivyo hivi sasa katika maeneo yote ya Zanzibar.
Aidha, Dk. Shein alisisitiza kuwa mafanikio hayo yote yametokana na uongozi bora wa ASP hadi hivi leo kuwa CCM, ambapo kwa kutambua umuhimu wa miundombinu ya barabara, ndipo imeweka kipaumbele hicho. AlIeleza kuwa kasi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeimarika zaidi, mara baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 tofauti na ilivyokuwa hapo kabla ya Mapinduzi hayo.
Dk. Shein aliongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni Serikali ya wananchi wote wa Zanzibar na kamwe hakuna Serikali nyengine, hivyo aliwataka wananchi kuendelea kuithamini Serikali yao na kuachana na wale wanaoibeza. Akieleza historia na umuhimu wa Mapinduzi, Rais Dk. Shein alisema kuwa kabla ya kuingia wakoloni wa Kireno, Zanzibar ilikuwa haikutawaliwa na badala yake iliongozwa na viongozi wenyeji wa kijadi wakiwemo Masheha, Maliwali, Madiwani na wengineo.
Aliongeza kuwa kukandamizwa, kunyonywa, kunyanyaswa pamoja na kunyimwa haki kwa Wazanzibari ikiwa ni pamoja na kunyimwa uhuru kutokana na ushindi wa kura za ASP kila pale uchaguzi unapofanyika ndiko kulikopelekea kufanyika kwa Mapinduzi ya Januari 12, 1964.
Katika hatua nyengine, Dk. Shein alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kumaliza ujenzi wa Barabara, kuanzia eneo la Fuoni Polisi hadi Tunguu.
FOLLOW US ON SOCIAL NETWORKS;
Instagram- https://www.instagram.com/ngwenjetv/
Facebook- https://web.facebook.com/mohamed.ngwenje
Youtube- https://www.youtube.com/channel/UCbzg...
website- https://ngwenjetv.wixsite.com/news
blogspot- http://ngwenjetv.blogspot.com/
Comments