Morogoro Watu watatu wakazi wa Chamwino Mnispaa ya Morogoro wanashikiliwa na Jeshi la polisi Mkoani Morogoro kwa tuhuma za kuhusika na mauji ya Boniface Kimbwansoni ambapo chanzo cha mauaji hayo kikitajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi. Taarifa ya Mwajuma Rambo kutoka mkoani Morogoro inasomwa studio ************************************************************************** Akizungumza na kituo hiki kwa njia ya simu kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kushikiliwa kwa watuhumiwa hao ambao ni Neema Godifrey ambaye ni mke wa Marehemu pamoja na mwanawe Alphoncina Bonfance ambaye ni mtoto na mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Kihonda pamoja na mtu mmoja ambaye jina lake halijatajwa kwa ajili ya upelezi.. SB Wilbroad Mutafungwa kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Kituo hiki kimefika eneo la tukio na kuzungumza na ndugu wa marehemu akiwemo Halima Mohamed shemeji wa marehemu na Costatino kanyasu mama mkubwa wa marehemu ambapo wameeleza hali ya maisha ya wanandoa hao kabla ya tukio hilo SB Halima Mohamedi shemeji wa marehemu Costatino Kanyasu mama mkubwa wa marehemu Kwa Upnde wake mjumbe wa mtaa huo Japhet Chogo amesema hilo ni tukio la kwanza katika mtaa huo na kuwaomba wananachi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi. SB Japhet Chogo mjumbe wa mtaa wa Mwande Mnaispaa ya Morogoro. Watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na upelelezi ukikamilika watafikiswa mahakamani. USISAHAU SUBSCRIBE NGWENJE TV, BONYEZA ALAMA NYEKUNDU ILIYOPO HAPO JUU HARAFU BONYEZA ALAMA YA KENGERE, BURUDIKA, ELIMIKA NA NGWENJE TV FOLLOW US ON SOCIAL NETWORKS; Twitter- https://www.twitter.com/ngwenjetv1/ Instagram- https://www.instagram.com/ngwenjetv/ Facebook- https://web.facebook.com/mohamed.ngwenje Youtube- https://www.youtube.com/channel/UCbzg... website- https://ngwenjetv.wixsite.com/news blogspot- http://ngwenjetv.blogspot.com/
top of page
bottom of page
Comments