MOROGORO Wadau wa Michezo mkoani Morogoro wamelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kutoa wataalamu watakaofatilia mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari (UMISETA) yanayoanza hivi karibuni katika ngazi ya mkoa, ili kuweza kutengeneza vijana wenye vipaji katika mchezo huo, watakaokuja kuitumikia timu ya taifa hapo baadae. Taarifa ya Mwajuma Rambo inafafanua Ni wachezaji wa timu ya Kombaini ya Manispaa ya Morogoro wakiendelea na mazoezi kujiandaa na mashindano ya UMISETA ngazi ya Mkoa, ambayo yanatarajiwa kuanza June Mosi mwaka huu, kwa kushirikisha halmashauri zote za mkoa wa Morogoro, mashindano ambayo yatatimua vumbi Wilayani Kilombero mkoani hapa. Katika kuelekea kwenye Mashindano hayo, wadau wa mchezo huo wamelishauri shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kuyatumia mashindano hayo kuanzia ngazi ya mkoa, kusaka vijana wenye vipaji, ambao watakuja kuzitumika timu za Serngeti na Taifa Stars hapo baadae. Vox Pops: 2 Emanuel Kimbawala-Mwalimu Mpira wa Miguu Leonard Komba-Mratibu wa UMISETA Kwa upande wao vijana wanaoenda kushiriki kwenye mashindano hayo, wamesema UMISETA ina umuhimu mkubwa kwa vijana wanaochipukia kwenye mchezo wa soka, kwani mashindao hayo yatawasaidia kuwatambulisha, na hata kuinua vipaji vyao. Vox Pops: 3 Selemani Iddy-Mchezaji Onesmo Samwel –Mchezaji Casian Yassint-Mchezaji Halmshauri zote za Mkoa wa Morogoro zitashiriki kwenye Mashindano hayo ya UMISETA, na baadae itaundwa timu moja, ambayo itauwakishilisha mkoa kwenye mashindano hayo kitaifa, ambayo kwa Mwaka huu yanatarajiwa kufanyika Mkoani Mtwara.
USISAHAU SUBSCRIBE NGWENJE TV, BONYEZA ALAMA NYEKUNDU ILIYOPO HAPO JUU HARAFU BONYEZA ALAMA YA KENGERE, BURUDIKA, ELIMIKA NA NGWENJE TV
FOLLOW US ON SOCIAL NETWORKS; Twitter- https://www.twitter.com/ngwenjetv1/ Instagram- https://www.instagram.com/ngwenjetv/ Facebook- https://web.facebook.com/mohamed.ngwenje Youtube- https://www.youtube.com/channel/UCbzg... website- https://ngwenjetv.wixsite.com/news blogspot- http://ngwenjetv.blogspot.com/ .
コメント