Serikali ya Tanzania na Rwanda kupitia Marais wake zimekubaliana kujenga reli ya kisasa (Standard Gauge) kutoka Kahama hadi Kigali. Jiwe la Msingi la Ujenzi wa reli hiyo linatarajiwa kuwekwa mwezi Disemba mwaka huu.
"Ujenzi wa Reli ya Kisasa kati ya Isaka, Tanzania hadi Kigali, Rwanda utasaidia kutengeneza ajira kwa wananchi wa nchi hizi mbili pamoja na kukuza na kuimarisha biashara na kufikia maendeleo tuliyoyaweka"-Rais @MagufuliJP
Comments