Na Merina Robert
Morogoro
LICHA ya jitihada zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau wengine katika kuhakikisha wazee wanapatiwa huduma bora ikiwemo ya afya lakini bado kundi hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutelekezewa watoto na kuwafanya kuwa wahudumiaji wakubwa wa familia hivyo kuchangia maisha duni kutokana na kipato kutotosheleza.
Wakizungumza na Clouds TV baadhi ya wazee wa mtaa wa Azimio kata ya Kihonda manispaa ya Morogoro akiwemo bi. Magreth Charles , bw. Wilson Karuwesa na mkurugenzi wa Shirika la Wazee Morogoro(MOROPEO) bw Samson Msemembo Wamesema wamekuwa wakipata shida katika kuhudumia familia kutokana na kutokuwa na kipato kinachotosheleza huku watoto walioachiwa wakitakiwa kupatiwa mahitaji muhimu ikiwemo chakula na mavazi.
Insert 01……..bi. Magreth Charles Mzee
Insert02 ……..bw. Wilson Karuwesa Mzee.
Insert03…..bw Samson Msemembo mkurugenzi shirika la wazee Morogoro(MOROPEO)
Katika kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wazee hao Shirika la HELPAGE linawasaidiaje wazee na hapa meneja miradi kutoka shirika hilo bw Joseph Mbasha anaeeleza mikakati ya shirika
Insert 04…….bw. Joseph Mbasha meneja miradi wa shirika la HELPAGE
shirika la HELPAGE kupitia Shirika la wazee mkoani Morogoro( MOROPEO) limefanya ziara ya kuwatembelea wazee katika mtaa wa azimio kata ya kihonda manispaa ya Morogoro ili kutambua changamoto zinazo wakabiri na jinsi ya kuwa saidia katika kutatua changamoto hizo
Comentários