halfan Diyu,
Taasisi ya michezo ya BS Promotion ya Morogoro,imeandaa bonanza la michezo wa ngumi ambalo litakuwa likifanyika kila siku ya Jumapili,ili kuinua na kuendeleza vipaji vya mabondia chipukizi wa Morogoro na wilaya zake.
akizungumza hivi karibuni mjini hapa na Ngwenje Tv,Mratibu wa Bonanza hilo ,Daudi Julian amesema bonanza hilo limeanza rasmi Februari 18 katika ukumbi wa Urafiki uliopo katika Kata ya Sabasaba,Manispaa ya Morogoro.
Julian amesema bonanza hilo litawashirikisha mabondia kutoka ndani na nje ya Morogoro,ili kuongeza ushindani na msisimko zaidi kwa wadau wa mchezo wa ngumi.
Mratibu huyo ameongeza kuwa taasisi hiyo imeamua kufanya bonanza hilo,ili kuibua ,kukuza na kuendeleza vipaji vya mchezo huo kwa vijana na wa Morogoro na nchi kwa ujumla.
"kama unavyofahamu ndugu mwandishi,mkoa wetu umejaliwa kutoa mabondia wazuri kama Francis Cheka na wengineo,hivyo inatubidi kuanza kutayarisha warithi wake ,kwa hiyo tunaamini katika bonanza hili tutapata vijana wazuri na wenye vipaji ambao watauletea mkoa wetu sifa na taifa kwa ujumla"amesema.
aidha Julian amebainisha kuwa katika bonanza hilo ambalo litakuwa likianza muda wa saa kumi jioni ,ili kuwapa nafasi mashabiki wengi kuhudhuria na kisha kuwahi kurudi majumbani kabla ya muda wa masaa ya usiku mkubwa,kutakuwa na kiingilio cha shilingi elfu mbili kwa kila mtu.
Opmerkingen