MAGAZETI FEB 12: Uamuzi wa Makonda Wazua Mjadala Uamuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wa kufuta mabaraza ya ardhi ya kata na wilaya, umezua mjadala mkubwa huku wadau mbalimbali wakieleza kwamba uamuzi huo ni kinyume cha sheria kwa sababu mabaraza hayo yaliundwa kisheria. Kwa upande wa uchaguzi wa ubunge wa Kinondoni, mgombea ubunge katika jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Salum Mwalimu ameanza kampeni za nyumba hadi nyumba kwa lengo la kuwashawishi wananchi wamchague. Akizungumza na Global TV, Salum Mwalim amesema ameamua kuzunguka nyumba hadi nyumba, ili kuwaonesha heshima wapiga kura wake kwa sababu anajua kutokanana majukumu, wengine hawana kabisa nafasi ya kuhudhuria kwenye mikutano ya kisiasa. Baada ya kampeni hiyo, Mwalimu amefanya mkutano mkubwa eneo la Kituo cha Polisi cha Ali Maua, Kinondoni jijini Dar es Salaam na kusindikizwa na makada wengine wakubwa wa chama hicho, ambapo amenadi sera za chama hicho
top of page
bottom of page
Comments