top of page
air
fa_edited
tangazo
1
2
ngwe6_edited
paul-kagame
majaliwa_edited
magufuri
makamu
Writer's pictureNgwenje Tv Report

Lwandamina atamka mazito


KOCHA Mkuu wa kikosi cha Yanga, George Lwandamina amesema kiwango kilichooneshwa na timu yake kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kimempa matumaini ya kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu.


Jumatano Yanga itakuwa mwenyeji wa Mwadui FC kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, mchezo ambao kocha huyo ameahidi kuchukua pointi zote tatu kutokana na maandalizi wanayoyafanya hivi sasa. Akizungumza na www.ngwenjetv.wixsite.com/news Lwandamina, alisema michuano ya Mapinduzi imemsaidia kuongeza ushindani wa kujituma uwanjani kwa wachezaji wake hicho ndicho kitu ambacho alikuwa anakitaka akiamini kila atakayepata nafasi atakuwa akicheza kwa bidii kuhakikisha anaendelea kucheza kikosi cha kwanza.


“Yanga hii haitegemei ukubwa wa jina, mchezaji ambaye ataonesha kujituma mazoezini ndiye atakayecheza mechi hata kule kwenye Kombe la Mapinduzi makocha waliopo ndiyo wametumia mfumo huo na mafanikio yameonekana,” alisema Lwandamina.Mzambia huyo alisema wanakwenda kuivaa Mwadui akijivunia maandalizi waliyofanya na ushindi kwao ni kitu cha muhimu kutokana na nafasi waliyopo hivi sasa, ambayo haiwaruhusu kuendelea kupoteza hata pointi moja.


Yanga imeshuka hadi nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi, kutokana na ushindi wa timu ya Mtibwa Sugar ambayo sasa imepanda hadi nafasi ya nne ilipocheza na Lipuli ya Iringa na kushinda bao 1-0.

3 views0 comments

Comments


bottom of page