KOCHA ST LOUIS; Yanga Ni Timu Nzuri BAO la mtokea benchi Juma Mahadhi limeipa Yanga SC ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Saint Louis Suns United ya Shelisheli katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mahadhi aliye katika msimu wake wa pili Yanga SC tangu asajiliwe kutoka Coastal Union ya Tanga, alifunga bao hilo dakika ya 66 kwa shuti akimalizia kona iliyopigwa na winga Geoffrey Mwashiuya iliyozua kizazaa langoni mwa Saint Louis. Mahadhi alifunga bao hilo dakika moja baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Ibrahim Ajib Migomba kama ilivyokuwa kwa mpishi wa bao lake, Mwashiuya ambaye naye alimbadili Emmanuel Martin
top of page
bottom of page
Comments