King Majuto amempongeza rais kwa kuongoza vyema.
- Ngwenje Tv Report
- Jan 31, 2018
- 1 min read
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, amemtembelea Muigizaji maarufu wa vichekesho nchini, King Majuto, aliyelazwa katika hospitali ya Muhimbili, anayeugua ugonjwa wa tezi dume. Baada ya kuonana na Rais Magufuli, King Majuto amempongeza rais kwa kuongoza vyema nchii hii na kuwa rais mwenye msimamo, huku akigusia suala la kutimua wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki.
Comments