GP Sirro Alivyomuapisha Kamishina wa Polisi Zanzibar Leo! MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro leo Februari 12, 2018 amemuapisha Kamishna wa Polisi (CP) Mohamed Hassan Haji kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar. CP Haji aliyeteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli hivi karibuni, pia amekula kiapo cha maadili ya uongozi wa umma mbele ya Katibu wa Viongozi wa Utumishi wa Umma, John Kaole. Akizungumza baada ya kumuapisha, IGP Sirro amemtaka CP Haji kushughulikia matukio yenye viashiria vya ugaidi na rushwa. “Viashiria vya ugaidi maana yake, kuna matukio kwa ndani ukiangalia kuna muelekeo wa ugaidi, unyang’anyi kwa kutumia sialaha kama ujambazi kama viashiria, ili tatizo ni la dunia nzima, kwa sababu haya yana tutia mashaka, ndio maana ninamuagiza hilo nalo aliangalie akiwa kule, haya matukio ya ujambazi ya ugaidi yakoje ili tuyashughulikie kwa pamoja,” amesema. Naye Katibu wa Viongozi wa Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma, John Kaole amemtaka CP Haji ajiepushe na vitendo vya ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa umma ili kusitokee mgongano wa masilahi. “Kazi zenu ni nyingi uwezekano wa kutokea kwa mgongano wa masilahi ni mkubwa, inabidi mjiepushe sana na ukiukwaji wa maadili kwa sababu unaweza kuleta mgongano wa masilahi lakini sina wasiwasi sababu mtazingatia kwa ukamilifu kwa sababu ni sehemu ya maadili ya maadili ya jeshi la Polisi,” amesema. Kwa upande wake CP Haji ameahidi kutekeleza maagizo ya IGP Sirro na kusema, “IGP ndiyo kiongozi wa juu kwenye jeshi letu ametoa maelekezo ya vipaumblele kwa hivyo vipaumbele hivyo mimi nitashughulikia yale maelekezo yaliyotolewa pale ili watanzania kwa ujumla na wazanzibar waishi kwa amani wapate haki zao wanavyostahili.” CP Haji alijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 1991 na kupandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Mkaguzi wa Polisi, Mrakibu wa Polisi, Mrakibu Msidizi wa Polisi na Kamishna Msaidizi wa Polisi.
top of page
bottom of page
Comments